Tiketi kwa ajili ya mechi ya kesho ya Simba na Yanga zimezua jambo jijini Dar kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakihaha kuzipata bila ya mafanikio.
Mashabiki wengi wa soka wamekuwa wakizunguka katika vituo vilivyotangazwa na Shirikisho la Ska Tanzania (TFF) kwamba vitaanza kuuza tiketi hizo lakini bila ya mafanikio.
Juhudi hizo za mashabiki hao zimewafanya waishie katika sehemu mbalimbali hadi katika ofisi za gazeti bora la Michezo la Championi.
“Tunazunguka kila sehemu, hatujui hizi tiketi zinauzwa wapi kwa kuwa kila kituo kinachoelezwa kuuza tiketi, hakiuzi,” alisema mmoja wa mashabiki.
Lakini baadaye Blogu hii ilifuatilia na kugundua tayari tiketi zilikuwa zimeanza kuuzwa katika maeneo haya Steers Posta, Benjamini Mkapa, Ubungo Oil Com, Buguruni Oil Com.
0 COMMENTS:
Post a Comment