Goli la Kaskazini kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam limeingia kwenye rekodi ya aina yake baada ya mechi ya
watani Simba na Yanga kwisha kwa sare ya mabao 3-3.
GOLI LILILORUHUSU MABAO SITA YA LEO |
Mabao yote sita ya mchezo huo kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo, yamefungwa kwenye goli hilo.
Yanga ndiyo walitangulia kufunga mabao
yao matatu kupitia kwa Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza katika kipindi cha kwanza.
Mabingwa hao watetezi wakaenda mapumziko
wakiongoza kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili, Yanga nao wakahamia
katika lango hilo na Simba wakafunga matatu kupitia Betram Mwombeki, Joseph
Owino na Gilbert Kaze na kuweka rekodi mpya.
Kwanza ni timu moja kusawazisha mabao
yote matatu na pili, lango moja kufungwa mabao sita katika mechi ya watani.
Lango hilohilo ndilo liliruhusu mabao matatu
kutinga wavuni wakati Simba ilipoifunga Yanga kwa mabao 5-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment