Vurugu kubwa zimeibuka wakati wa mechi ya
Bara kati ya wenyeji Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Vurugu hizo zimetokea mara tu baada ya
mwamuzi kupuliza kipyenga kuashiria mpira kwisha mara tu baada ya Kagera Sugar
kupata bao la kusawazisha lililofungwa na beki Salum Kanoni kwa mkwaju wa
penalty.
Mashabiki wa Simba walianzisha vurugu
wakipinga mwamuzi kutoa penalty hiyo ikiwa ni baada ya Simba kufanikiwa kupata
bao katika dakika ya 44 mfungaji akiwa Amissi Tambwe.
Bao hilo lilidumu hadi mapumziko na
kipindi chote hakukuwa na bao hadi wakati wa dakika za nyongeza, Paul Ngwai
alipoangushwa kwenye eneo la hatari.
Matokeo hayo ya bao 1-1 yalionyesha
kuwakera mashabiki walioanzisha vurugu hizo, wakivunja viti hali iliyosababisha
askari uwanjani hapo watupe mabomu ya machozi na amani ikapotea.
Baadhi ya watu walizimia na wengine
kuumia na watu wa Msalaba Mwekundu wakaanza kutoa huduma ili kuokoa maisha yao.
0 COMMENTS:
Post a Comment