October 31, 2013

KABANGE

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mlage Kabange amemuambia bosi wake wa zamani, Abdalla Kibadeni  asitegemee mchekea katika mechi ya leo.

Kagera Sugar watakuwa wageni wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kuendelea kusaka pointi tatu muhimu za Ligi Kuu Bara.

Kabla ambaye alikuwa msaidizi wa Kibadeni wakati akiwa Kagera Sugar, amesema wamejiandaa vizuri na Simba wategemee mechi ngumu na ikiwezekana kupoteza.

“Najua Simba watakuwa wazuri kwa kuwa wana kocha mzuri, lakini lazima wapate upinzani mkali na kweli sisi tunataka kushinda.


“Kibadeni ni kocha mzuri na alipokuwa Kagera ameniachia urithi wa baadhi ya mambo muhimu. Lakini leo kila mtu atakuwa kazini na kutaka kushinda,” alisema Kabange ambaye pia ni mchezaji nyota wa zamani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic