Kampuni
inayoongoza duniani kwa kutengeneza vifaa
bora vya Elektoniki--Sony, imeendeleza
dhamira yake ya kuleta mageuzi ya kiteknolojia Tanzania, na safari
hii imezindua vifaa
vya kisasa vyenye matumizi
rahisi katika soko
la bidhaa hizo nchini.
Sony,
inayoongoza kwa kupendwa na wanamichezo maarufu na watu wengine mbalimbali, pia katika
soko la kimataifa ya
vifaa vya Kielektroniki, imezindua Kamera
tatu za kisasa
na televisheni kubwa ‘Sony Bravia Full HD 3D LED TV W8 Series’.
Kamera
zilizozinduliwa kwa lengo
la kuleta mageuzi ya kiteknolojia nchini, ni Video Camera
Sony Handycam HDR-PJ380
camcorder, Kamera ya
picha za mnato Cyber-Shot
HX300 digital still camera
na runinga ya kisasa kwa matumizi
ya nyumbani (Home
Cinema System- BDV-N9900SH).
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa vifaa hivyo, mwakilishi
wa Sony kwa
nchi za Mashariki ya
Kati na Afrika,
Rajeev Pallippamadam alisema uzinduzi wa
vifaa hivyo nchini
Tanzania, unathibitisha
dhamira ya Sony kuwekeza
vifaa vya kisasa
katika soka la Kielektroniki.
“Kama
Kampuni, Tanzania ni
moja ya kielelezo cha
awali katika soko
la vifaa vyetu. Leo
tunataka kuwekeza uzoefu wa
matumizi ya vifaa
hivi, tukitegemea kuwa watumiaji
watapata fursa nzuri na
pana katika kutanua
wigo wa uelewa wa
vifaa vya Sony,”
alisema Pallippamadam.
Uzinduzi
wa vifaa hivyo
ni sehemu ya mikakati
ya Sony kujikita
zaidi katika kuwekeza soko
la vifaa vyake
barani Afrika, ambapo imepanga
kuongeza mtaji mara mbili
kufikia Dola Bilioni
1.5 mpaka mwaka 2015.
0 COMMENTS:
Post a Comment