October 7, 2013



 
MICHAEL AKICHUANA NA MWOMBEKI
 Beki tegemeo wa kati wa Ruvu Shooting, George Michael amekiri kwamba mziki wa mshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki ni kiboko.


Michael amesema kati ya washambuliaji wenye nguvu ambao amewahi kukutana nao ni Mwombeki.

Wawili hao walikutana wakati timu hizo zilipotoka sare ya mabao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumamosi.

“Kweli yule jamaa yuko fiti sana, alinipa wakati mgumu kuliko nilivyotegemea,” alisema.

Wakati Michael alikuwa akihofiwa na wachezaji wa Yanga wiki moja timu hizo zilipokutana, mara kadhaa alijikuta akienda chini alipopambana na Mwombeki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic