Algeria imefanikiwa kufuzu kucheza Kombe la
Dunia mwakani nchini Brazil baada ya kuichapa Burkina Faso kwa bao 1-0.
Kwa ushindi huo, timu hizo
zimelingana mabao 3-3, lakini Algeria iliyokuwa nyumbani imepata advantage ya
mabao ya ugenini baada ya kufungwa 3-2 katika mechi ya kwanza ikiwa ugenini.
Algeria imekuwa timu ya kwanza ya
Afrika Kaskazini kusonga mbele baada ya timu tatu za kwanza, Ghana, Nigeria, Cameroon na
Ivory Coast zote kuwa zinatoka Afrika Magharibi.
Bao pekee la mchezo wa leo lilifungwa
na Bougherra katika dakika ya 49.
Wageni walicharuka mwishoni, hata
hivyo walikosa nafasi zaidi ya mbili ambazo kama wangefunga hata bao moja maana
yake wangesonga.
0 COMMENTS:
Post a Comment