November 3, 2013


Mashabiki wa Manchester United wamekasirishwa na kitendo cha kiungo wa Fulham, Sascha Riether kuonekana akiwa amevaa jezi ya timu hiyo halafu ametabasamu.
 
Riether  ndiye aliyemkanyaga kwa makusudi kinda hatari wa Manchester United, Adnan Januzaj wakati United ilipoitwanga Fulham kwa mabao 3-1, jana.


Alimkanyaga kinda huyo kwa makusudi, lakini baadaye akaonekana akiwa ni mwenye furaha kubwa na jezi ya Man United ambayo alibadilishana na mchezaji mmoja wa United baada ya mechi.


Baadhi ya mashabiki wa United waliochangia kwenye akaunti ya klabu hiyo kwenye mtandao wa Twitter, wameponda wakisema mchezaji huyo ‘katili’ hakupaswa kuvaa jezi ya timu yao.

Asilimia kubwa ya mashabiki walimuita mnafiki na muumizaji kwa makusudi, hivyo hakupasswa hata  kupewa jezi ya timu yao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic