February 8, 2020



UONGOZI wa Simba umesema kuwa umefungwa na timu iliyokuwa bora ndani ya Ligi Kuu Bara.


Simba ilifungwa bao 1-0 na JKT Tanzania kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru, jana, Februari 7,2020 lililopachikwa kimiani na Adam Adam dakika ya 24 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wamefungwa na timu iliyokuwa bora ndani ya uwanja.

"Tumefungwa na timu bora, hakuna cha kukata tamaa bado mapambano yanaendelea,".

Simba imepoteza jumla ya mechi mbili ndani ya ligi kati ya 20 ambazo imecheza kwa sasa na zote imepoteza kwa kufungwa bao moja.

 Iliianza kufungwa mbele ya Mwadui FC bao 1-0 mzunguko wa kwanza na safari hii imefungua mzunguko wa pili kwa kichapo cha bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania.

16 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Tafuta neno lingine la kiushabiki. Hili la makocha huwezi kujua wa nani atawahi kuondoka. Kuzishabikia hizi timu inahitaji uzifahamu zilivyo.

      Delete
  2. Leo najua mko busy mnafanya njia zote chafu ili Yanga afungwe ili muwazibe mdono mashabiki ili muendelee kupiga mpunga hapo clubuni. Ukweli unabaki timu ya Simba ni mbovu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio kweli. Huko ni kuwadharau Ruvu Shooting. Kuwa na heshima timu zote zinashindana katika ligi. Si Simba na Yanga pekee. Kufungwa Simba si ajabu ndio maana ikaitwa ligi. Mshindi anapatikana baada ya mechi 38.

      Delete
    2. Sasa harufu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo huwa zinatoka wapi?

      Delete
    3. Nani amethibitisha hio harufu? Na alichukua hatua gani? Hizi timu zetu zinajua zinapata presha kwa mashabiki kwahio wanaishi na visingizio ikitokea matokeo sio mazuri kwao.

      Delete
  3. Hivyo visingizio hadi vita,nkana na timu zote club bingwa zilizokua zinalalamikia harufu zilikua zinatafuta sababu baada ya kufungwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi unaelewa seriousness ya ishu unayoandika? Tuache maneno ya mtaani. Sijawahi kusikia Simba kupigwa faini na CAF ama TFF kuhusu suala hilo. Zaidi wote wamekiri kuzidiwa kimchezo.

      Delete
    2. Yaani mpigwe tano ugenini tena za kuhurumiwa arafu mje kushinda Taifa!! Ilikuwa haingii akilini sana. Kama ndio hivo mpira sio Science. Kama ndio hivo timu ya taifa ya ujerumani wakija hapa tunaweza kuwafunga.

      Delete
    3. Hio ndio soka na zaidi soka la kiafrika. Yanga walitoa sare ya 3-3 na Raja Casablanca lakini ikaruhusu kufungwa goli 6 Morocco katika ligi hiohio ambayo Simba imefungwa tano. Kwahio hoja hiyo haina mashiko.

      Delete
  4. Washabiki wa soka tuwe na ushahidi kila tunapoandika mambo makubwa kama haya ya kupuliza dawa vyumbani.
    Hii ni jinai kubwa kama ikithibitika. Lakini ni jambo linalohitaji uchunguzi mkubwa wa kina.
    Simba wamewahi kutuhumiwa na AS Vita katika jambo hilo, lakini Yanga pia waliwahi kutuhumiwa na baadhi ya timu, wakiwemo Zanaco ya Zambia walipokuja kucheza mechi ya Ligi ya mabingwa wa Afrika mwaka 2017.
    Mbao FC na Toto African wakati wanacheza wote Ligi Kuu jijini Mwanza wamewahi kutuhumiana katika uchafu huo, na wanaohifadhi kumbukumbu wanajua kwamba hata Stand United wamewahi kuingia kwenye lawama hizo.
    Hata hivyo kwakuwa hakuna ushahidi ni mambo yanayohitaji uchunguzi makini sana.
    Rai yangu ni kwamba ushauri wetu ulenge kusaidia maendeleo ya soka, na yale ambayo hatuyaoni kwa macho tusiyape nafasi katika mawazo yetu.

    ReplyDelete
  5. Southampton alifungwa goli 9 nyumbani na Leicester kwenye ligi tarehe 25 nov 2019.Tarehe 11 januari 2020 Leicester akafungwa 2-1 na Southampton nyumbani kwa Leicester .Kwenye mpira matokeo kama haya hutokea. Ndio maana watu kusema mpira unadunda. Hakuna maajabu.

    ReplyDelete
  6. Mi nashangaa mnavyopata tabu kuwaeleimisha watu ambao kisaikolojia wanajua kufikia mafanikio ya simba ni ndoto kwao kwa hiyo lazima wazushe hoja za kuonesha Simba hawakuwa na uwezo wa kufika robo fainali, wamechukua ubingwa wa Tanzania mara 27 km wangekuwa wanachukua kihalali mana yake michuano ya Afrika wangekuwa na rekodi nzuri kushinda Simba kwa kuwa wameshiriki mara nyingi lkn Simba(mara 20)amefika fainali ya CAF mwaka 1993 Je walikuwa wanapulizia dawa kipindi hicho, roho zinawauma sana ukweli ni kwamba nyinyi ndio timu iliyobebwa zaidi toka mpira umeanza nchi hii (Ndolanga, Malinzi )mmesahau Simba ndo bingwa mara nyingi michuano ya kagame huko hakuna akina ndolanga na Malinzi,Al ahly alietufunga sisi tano nae alipigwa tano na Sundowns na yeye alikuwa anapulizia dawa, hamkumbuki hata tulivyowapiga (5 -0)walisema eti kwa sababu wazee wao walivua kofia hawa watu hawaamini ktk kucheza mpira ni uchawi na visingizio kama hivyo visivyo na tija nnachijua mimi mtu akikwambia akili zako kama mshabiki wa Yanga pigana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tunashukuru maelezo haya marefu inaonyesha hiki kitu ni kibaya. Na ubaya zaidi unakuja pale kitimu kichanga kama Namungo nacho kinafanyiwa.

      Delete
    2. Itawauma sana safari hii msimu wa tatu hakuna ubingwa. Mtabaki na stori za magazetini.

      Delete
    3. We unashangaa Namungo hata kitimu kidogo kama Ruvu Shooting ilibidi kishinde mbili bila (2 - 0)lakini refa moja akalikataa goli dhahiri kabisa dhidi ya Yanga

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic