Hakuna aliyekuwa akifikiri kwamba
mshambuliaji kutoka nchini Burundi atakuwa tishio katika katika Ligi Kuu Bara
hasa kwa upachikaji wa mabao.
Lakini sasa Amiss Tambwe wa Simba, raia
wa nchi hiyo ndiye anasumbua huku kukiwa na Mrundi mwingine, Didier Kavumbagu
wa Yanga pia akionekana kuwa na ubora mzuri.
Mpira una mambo mengi sana, wakati
mwingine hisia zinachukua nafasi zaidi kuliko hali halisi, kama kipindi ambacho
Yanga walikuwa wakiamini washambuliaji Wakenya ndiyo wanaoweza kuifanya timu
hiyo ing’are.
Kumbukia wakati wakiichezea akina Ben Mwalala,
Maurice Sunguti au Boniface Ambani. Lakini leo Mganda anaweza kufanya vizuri
akiwa katika kikosi hicho.
Hisia za mashabiki au hata walaamu wa
soka zinaendana kwa karibu kabisa bila ya kujali ni nchi gani. Ulaya pia mambo
hayo yamekuwa yakitokea, wao wanaona ni imani wala si uchawi.
Hivi karibuni kumeibuka mjadala mkubwa
kuhusiana na kiungo wa Real Madrid, Gareth Bale kutokea Wales ambayo ni nchi ya
asili ya Kingereza.
Kwamba pamoja na kununuliwa kwa gharama
kubwa zaidi ya pauni milioni 86 na Real Madrid lakini hawezi kuwa staa zaidi na
badala yake atabaki kuwa chini ya Ronaldo.
Wachambuzi wa jarida moja maarufu la
michezo wamechambua pia na kusema Bale ataendelea kubaki namba mbili au tatu
kwa ubora katika kikosi cha Madrid.
Wachambuzi hao wamerudia nyuma kama
ambavyo Watanzania wamekuwa wakiamini mambo tofauti katika michezo, mfano
kuamini kutokana na uraia au nchi anayotokea mtu fulani.
Uchambuzi huo unaonyesha hivi, wachezaji
wengi kutoka nchi za Kingereza hawajawahi kuwa nyota katika La Liga namba moja
katika wakati husika na hasa kama wamesajiliwa na Real Madrid na hiyo inatokana
na aina ya uchezaji wao, hata kama watakuwa bora kiasi gani.
Mfano unatolewa wa Steve MacManaman,
Michael Owen na David Beckham ambao walitokea England wakiwa nyota wakubwa
kwao, lakini Hispania wakashindwa kuwapiku Rau Gonzalez, Figo, Zinedine Zidane
na Ronaldo de Lima.
Hali hiyo imeonekana kama ni ushindani
wa kitaifa, kwani vyombo vya habari vya nchi za Kingereza zimeonyesha kupingana
vikali na namna vyombo vya habari vya Hispania na hata Ureno vinavyochambua.
Baadhi ya wachambuzi wa Uingereza pia
wameingia katika hilo na kuonyesha Bale atazima hayo yanayosemwa wakiyaona kama
ni zimwi linaloshindika na mwisho mapinduzi yanapatikana.
TAKWIMU
MECHI MABAO
PASI
4 3 4
0 COMMENTS:
Post a Comment