Na
Mwandishi Wetu
Mashabiki wa Simba na Yanga kwenye
miji ya Shinyanga 'Shy Town' na Moshi watapambana vikali na kuburudika katika michezo
mbalimbali kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe lililoandaliwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager litakalofanyika uwanja wa Shycom mjini Shinyanga na
uwanja wa CCM Mkoa mjini Moshi siku ya Jumapili wikendi hii.
Mratibu wa mabonanza hayo Lawrence
Andrew, amesema kuwa michezo mbalimbali ikiwemo soka bonanza la wachezaji saba
kila upande, kuvuta kamba, na pia mpira wa mezani maarufu kama fussball
itapamba mabonanza hayo. Burudani mbalimbali pia zitapamba bonanza
litakalofanyika Moshi zikiwemo burudani ya muziki kutoka bendi ya Malindi Band
pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa mkoani Kilimanjaro.
Michezo kama hiyo pia itakuwepo
kwenye bonanza litakalofanyika Mkoa wa Shinyanga ambapo bendi maarufu mkoani
humo ya TMA Band itatoa burudani kabambe kwa mashabiki watakaojumuika kushiriki
bonanza hilo pamoja.
Andrew pia amesema kuwa vilevile kuwa
michezo mbalimbali ya kujifurahisha kama vile kufukuza kuku wa kienyeji,
kukimbia na gunia na kupiga penati ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba
mabonanza hayo ambayo yatafanyika katika mikoa hiyo kwa mara ya kwanza kupitia
Nani Mtani Jembe. Kampeni hii ya aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa
mashabiki hao kujumuika pamoja na kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya
ushindani na utani wa jadi kati ya mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee
kuonyesha mapenzi kwa timu zao.
Mabonanza hayo yanalotarajiwa kuanza
saa tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo
ilizinduliwa Oktoba 2 na inafanyika nchi nzima ikiwashirikisha
mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia kampeni hiyo, Kilimanjaro
Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi
milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi
milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George
Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa
kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha
nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe
alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa
shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga
anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye
kizibo chake kuna namba ya kushiriki.
Alisema baada ya shabiki kununua bia
ya Kilimanjaro Premium Lager na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa
kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno
akianza na jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo
na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema baada ya shabiki kutuma namba
hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa
shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi
10,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa
amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.
Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya
uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi
siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment