Uongozi wa Klabu ya Coastal Union, umesema unamtaka kocha mpya wa timu hiyo, Yusuf
Chippo, ahakikishe anaipa mafanikio msimu huu.
Coastal
imemchukua kocha huyo kwa mkataba wa miaka miwili, baada ya kulitimua benchi
lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco.
Hatua
hiyo imechukuliwa kutokana na kufanya vibaya katika michezo ya Ligi Kuu Bara,
wakati viongozi wakiamini wana kikosi cha kutwaa ubingwa.
Katibu Mkuu wa Coastal, Kassim el Siag, alisema
wanamtaka kocha huyo ambaye ni raia wa Kenya awape mafanikio ya kumaliza katika
nafasi za juu.
Alisema
hawana hofu naye kwa kuwa anaijua timu hiyo na alikuwa akihudhuria kwenye mechi
zao mbalimbali za ligi kuu walizokuwa wakicheza.
“Ukiangalia
tuna pointi chache sana, 16, tupo nafasi ya nane, hivyo tunataka kuona anatupa
mafanikio, hiyo itamsaidia na yeye kujiongezea CV (wasifu) yake,” alisema el
Siag.







0 COMMENTS:
Post a Comment