Kura za mashabiki ndizo zitakazomfanya mwakilishi wa Tanzania katika
shindano la Project Fame, Elisha Maghiya maarufu kama Hisia aendelea kupeta.
Kazi hiyo imeanza leo, kufuatia washiriki wa shindano la Tusker
Project Fame kuanza kuchujwa kwa kufuata wingi wa kura kutoka kwa mashabiki,
watanzania na mashabiki wa shindano hilo.
Kwa ujumla
wanaombwa kumpigia kura Elisha Maghiya (Hisia) mtanzania pekee aliyebaki katika
shindano hilo kwa kutuma neno TUSKER 12 kwenda namba 15324 na pia kupiga kura
kupitia www.tusker.mob
kwani hata akiimba vizuri sana bila kura nyingi zaidi atashindwa kuendelea
kuiwakilisha nchi yetu katika shindano hilo.
Kufuatia
washiriki kuchuana vilivyo huku kila mmoja akionesha kuwa mkali Zaidi, majaji
walijikuta wakishindwa kuchagua ni nani kuingia kikaangoni kwa wiki mbili
mfululizo, hivyo kuamua kuwa kwa sasa utaratibu utabadilika na washiriki
watatolewa kulingana na idadi ya kura zitakazopigwa na mashabiki wa shindano
hilo.
Mshiriki
mwenye kura chache atatolewa katika mashindano hayo. Hivyo kufuatia hali hiyo
kila mshiriki anategemea mashabiki wake kumuokoa.
Naye meneja
wa bia ya Tusker kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti, Saialouise Shayo
amewasisitiza Watanzania na mashabiki wa shindano la Tusker Project Fame
kumpigia kura mshiriki pekee kutoka Tanzania aliyebaki.
“Hisia
ameonesha jitihada kubwa sana katika kuhakikisha anautwaa ushindi wa shindano
hilo hivyo tusimuangushe kwani kwa sasa ni kura za watanzania na mashabiki kwa
ujumla zitakazomfanya aendelee kufanya vyema katika mashindano ya Tusker
Project Fame,” aliongeza Shayo.
Wiki
iliyopita Hisia aliimba wimbo wa ‘Big Bad Wolf’ huku akionesha kujiamini na
tabasamu zito kama kawaida yake na kuwafanya mashabiki na majaji waridhike na
uimbaji wake.
Hisia
alitawala jukwaa baada ya Patrick kuimba wimbo wa ‘Nchi Ya Kitu Kidogo’
ulioimbwa na Eric Wainain. Pia alifuatiwa na Nyambura ambae alihitimisha
simulizi ya hadidhi yao kwa wimbo wa ‘My Immortal’ ulioimbwa na Evanescence,
kwani washiriki hao waliimba nyimbo zao katika staili ya kutoa kisa
kinachokamilisha hadithi.
Jumamosi
iliyopita washiriki waliimba nyimbo kutokana na uchaguzi wa majaji. Hii
ilitokana na kutokuwepo kwa mshiriki yeyote kikaangoni kwa wiki iliyopita.
Hisia alitumbuiza wimbo wa ‘Radioactive’ ulioimbwa na Pentatonix, huku
akishirikiana na Amosi na Nyambura wote kutoka Kenya.
Wimbo huo
ulikuwa ni chaguo la jaji Ian. Mashabiki na majaji walifurahishwa na uimbaji wa
Hisia na kumfanya aendelee kujiwekea nafasi nzuri katika mashindano hayo.
Usikose
kufuatilia mashindano haya yanayorushwa kupitia televisheni ya East Afrika TV
siku ya jumapili kuanzia saa moja na nusu usiku pamoja na jumamosi kuanzia saa
mbili usiku, pia televisheni ya ITV kuanzia saa nne kamili usiku siku ya
jumamosi na jumapili.
0 COMMENTS:
Post a Comment