November 1, 2013

YAHAYA

Mwenyekiti mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yahaya Mohammed amesema anataka kuzungumza na viongozi wote wa timu za ligi na ataanza na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.


Yahaya amesema anaamini kuwa ushirikiano na viongozi wa ligi kuu ndiyo utawafanya wafanikiwe na kwanza ataanza na Manji.

Mwenyekiti huyo ambaye alichaguliwa Ijumaa iliyopita, alisema atamfuata Manji ofisini kwake ili azungumze naye na atoe mchango wake kwa ajili ya maendeleo ya ligi.

“Ukweli nataka kukutana na viongozi wote wa ligi kwa ajili ya kuzungumza nao kwa ajili ya kupata mchango wao kwenye ligi.

“Lakini nafikiri kuwa nitaanza na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, naamini ana mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya soka letu.


“Naamini kuwa tukishirikiana basi tunaweza kuuendeleza mchezo wetu wa soka, lakini baada ya kumalizana na Manji basi nitahamia kwenye klabu nyingine za ligi na kuzungumza na viongozi wao,” alisema Mohammed.

Yanga imekuwa ikipinga kupewa Sh milioni 100 sawa na klabu nyingine kwa kuwa yenyewe ni kubwa.

Klabu hiyo kongwe imekuwa ikitaka utumike mfumo kama ilivyo Hispania, England na kwingineko ambako haki za TV hulipwa kulingana na wingi wa mashabiki wanaofuatilia timu fulani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic