Kiungo mshambuliaji wa Kilimanjaro
Stars, Mrisho Ngassa, ametengeneza staili mpya ya nywele atakayoitumia kwenye Michuano
ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya.
Nyota
huyo mwenye kasi uwanjani akiwa amenyoa staili ya kiduku huku pembeni akiwa
amepaka ‘brichi’ ya rangi ya khaki wakati Stars ikiivaa Zambia na kutoka nayo sare ya bao 1-1.
Ngassa ambaye amezoeleka kuonekana
akiwa amenyoa kiduku muda mwingi, sasa hivi ameamua kuongeza mvuto zaidi
kichwani mwake kwa kuweka rangi hizo.
Pamoja na Ngassa kupaka rangi wachezaji wengine wa Stars, Said Morad na Kelvin Yondani walikuwa wamepaka rangi hizo pia.
.jpg)







0 COMMENTS:
Post a Comment