Mashabiki wa Simba wamejitokeza kwa
idadi ndogo sana leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Furaha ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya
Ashanti United imeshangiliwa na mashabiki wachache wengi wakiwa na hofu ya
kukamatwa na Jeshi la Polisi kutokana na ung’oaji wa viti.
Mashabiki wa Simba waling’oa viti katika
mechi waliyotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar wakimtuhumu mwamuzi
kuwanyonga.
Tayari Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa
Temeke, linawashikilia mashabiki 11 ambao wanatokea katika vikundi mbalimbali
vya ushangiliaji.
Katika mechi ya leo, mashabiki hasa
vikundi hivyo walikuwa wachache na ilionekana ni hofu kubwa ya kuingia katika
mtego wa polisi kama ilivyokuwa kwa wengine 11 waliokamtwa leo.







0 COMMENTS:
Post a Comment