November 16, 2013


Ronaldo ameonyesha yeye ni kati ya wachezaji wakubwa na muhimu baada ya kuifungia Ureno bao pekee katika mechi ya mtoano kuwania kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Sweden iliyokuwa inaongozwa na Zlatan Ibrahimivic.


Ureno imeshinda bao 1-0 na hivyo inasubiri mechi ya marudiano wiki ijayo nchini Sweden.

Angalau Ureno ambayo katika michezo ya kuwania kucheza Kombe la Dunia ilikuwa inasuasua, imeamsha matumaini.




Ronaldo alifunga bao hilo katika dakika ya 83 huku wengi wakiwamini mpira ulikuwa umemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Wareno wengi walikuwa na hofu kwa kuwa Sweden walionekana kuwa bora zaidi na walishambulia na kukosakosa zaidi.

Maana yake, lazima Wareno wacheze vizuri zaidi wakiwa ugenini ili kujihakikishia kusonga hadi Kombe la Dunia.






Portugal: Patricio, Pereira, Coentrao, Veloso, Pepe, Regufe Alves, Meireles (Josue, 78), Moutinho, Postiga (Almeida, 66), Nani, Ronaldo
Subs not used: D Carvalho, R Carvalho, Pereira, Na Bangna, Moreira da Costa, Neto, Varela, Antunes, Bastos Pimparel, Macedo Lopes
Goal: Ronaldo 82
Booked: Pereira, Ronaldo
Sweden: Isaksson, Lustig, Olsson, Elm (Wernbloom, 72), Nilsson, Antonsson, Larsson, Kallstrom (Svensson, 77), Ibrahimovic, Elmander (Gerndt, 88), Kacaniklic
Subs not used: Olsson, Wiland, Granqvist, Bengtsson,  Johansson, Toivonen, Durmaz, Zengin, Nordfeldt
Booked: Larsson, Elmander

Ref: Nicola Rizzoli

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic