November 16, 2013


Nimeikuta hii picha kwenye wall ya facebook ya Mwani Nyangasa, dada na mshikaji. Nimefurahi sana kwa kuwa sina picha bora kama hii nikiwa kazini, badala yake nimekuwa nikiwapiga wengine tu.


Nimefurahi sana, hehe. Kumbe namna hii ndiyo hufanya kazi, nasikia raha kwa kuwa ndiye kiongozi pekee wa gazeti ambaye amekuwa akipiga picha, bosi wa wahariri anayeweza kukubali kwenda mtaani kutafuta stori na kupiga picha.

Wakati mwingine wahariri ambao mimi ni bosi wao, hunipa kazi ya kupiga picha, ninaenda na kurudi na kazi safi kabisa.

Ninaamini hata wengine wanaochipukia au wale wakongwe wanaweza kujifunza katika hili. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa uwezo mzuri alionipa, kila kukicha nang’amua mengi na ninaendelea kujifunza. Daima siwezi kuvimba kichwa kwa kuwa kama ni hivyo, ningekuwa nimepotea siku nyingi.

Kama ningekuwa mjinga ningevimba kichwa kwa kuwa nimefanya mengi sana katika uandishi wa michezo na wengi hawajafikia. 

Mahojiano na wachezaji wengi wakubwa kama Kolo Toure, Yaya Toure, Didier Drogba, Steven Pierneer, Samuel Eto’o, Salmon Kalou, Emmanuel Ebou na wengine wengi ambao hata nimesahau.

Makocha kibao kama Pitso Mosimane, Gareth Southget, Sabri Lamouch, Marcelo Lippi, Dunga na wengine wengi tu lakini hadi leo niko kawaida na ninaendelea kupiga kazi kama zamani.
Nashukuru kwa kujitambua, nakushukuru Mwani kwa picha nzuri. Ahsante mnaoniunga mkono kwa kunisapoti, siku zote napokea changamoto na ushauri. 

AHSANTE SANA MUNGU KWA YOTE HAYA.
Aluta continua.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic