November 6, 2013

MWOMBEKI KATIKA MOJA YA MECHI ZA SIMBA

Simba imeitwanga Ashanti United kwa mabao 4-2 katika mechi tamu ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.


Vijana hao wa Msimbazi ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 8 kupitia kwa Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye aliwachambua mabeki, lakini Ashanti wakaonyesha ni wabishi kwa kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 45 kupitia Hussein Sued.

Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa sawa, lakini kipindi cha pili, Simba walionyesha uhai mapema na kupata bao la pili katika dakika ya pili tu tokea kuanza kwa kipindi hicho, safari hii Mrundi, Amissi Tambwe akitikisa nyavu tena.

Dakika ya 49 ambayo ilikuwa ni tatu tatu tu tokea Tambwe afunge, Betram Mwombeki akafunga bao la tatu lakini Ashanti wakajibu mapigo dakika ya 52, mkongwe Said Maulid ‘SMG’ akionyesha uwezo wake.


Ikionekana kama Ashanti wangeweza kufanya matokeo hayo kuwa sare, Simba walipata bao la nne na  katika dakika ya 89, Ashanti wakapata ‘kimeo’ baada ya kipa wao Amani Simba kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kudaka mpira nje ya eneo la 18, Daud Mwasongwe akingia kulinda lango baada ya Paul Maono kutolewa ili aweze kuingia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic