Mashindano ya mchezo wa riadha ya
Kilimanjaro yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar lakini habari njema ni kuongezwa
kwa zawadi kwa washindi.
Meneja wa Kampuni ya Bia ya
Kilimanjaro George Kavishe ambao ndiyo wadhamini wakuu amesema katika mbio hizo
ambazo pia zitawahusisha watu wenye ulemavu zawadi za safari hii zimeongezeka
kwa asilimia 25 ambapo pia kwa Mtanzania yoyote atakayebahatika kuvunja rekodi
atazawadia kiasi cha Sh mil 2 zaidi ikiwa kama motisha.
“Tunataka kuona ushindani unaongezeka
safari hii ndiyo maana Kilimajaro ikaongeza kiwango cha zawadi tofauti na msimu
uliopita, lakini pia hatujawasahu Watanzania nao tumewaka kuhakikisha wanajituma
na endsapo yoyote atabahatika kuvunja rekodi atapata kiasi cha Sh milioni mbili
zaidi kama motisha,” alisema Kavishe.
Mbio hizo zilizoanzishwa mwaka 2003
zimezinduliwa rasmi mgeni rasmi akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni,Vijana na Michezo Elisante Ole Gabriel katika hafla fupi ilifanyika
katika Hoteli ya JB Belmonte.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na
wawakilishi wa makampuni mbalimbali wa mashindano hayo yatakayofanyika Machi 2
2014 mwakani Ole Gabriel amewasifu waratibu wa mbio hizo kwa kufanya jitihada
za kudumisha mbio hizo ambapo zinachangia kukuza sekta ya utalii nchini.
“Takwimu zinaonyesja kwamba takribani
raia mbalimbali duniani hushiriki mbio hizi ambao wanatoka Mataifa zaidi ya
arobaini duniani, hilo pekee linaleta picha ya kwamba sekta ya utalii
inaimarika, niseme kwamba kama kuna lolote mtalihitaji kutoka wizarani msisite
kutujulisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment