November 12, 2013




Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitawavaa Kenya, Harambee Stars katika mechi itakayochezwa Novemba 19 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Rais wa Shirikisho la Kenya (KFF), Sam Nyamweya amethibitisha kuwepo kwa mechi hiyo ya kirafiki iliyo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataida (Fifa).

Akizungumza na SALEHJEMBE jijini hapa, Nyamweya alisema mechi hiyo ya kujipima nguvu itakuwepo baada ya mashirikisho hayo mawili kukubaliana.

“Nimezungumza na Rais Malinzi wa TFF, kila kitu kimekubalika na sasa mechi hiyo itachezwa Dar es Salaam,” alisema Nyamweya.
 
NYAMWEYA (KULIA) AKIWA NA AMROUCHE
Awali kulikuwa na taarifa mechi hiyo ingechezwa jijini Arusha lakini Kocha Mkuu wa Harambee Stars, Adel Amrouche akaukataa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kuwa ni mbaya.

Kweli saa chache baadaye tokea kocha huyo aukatae uwanja, Bodi ya Ligi Kuu ikatangaza kuufunga kwa madai hauna hadhi na hasa katika sehemu ya kuchezea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic