November 13, 2013



Kikosi cha Taifa Stars leo kimecheza mechi mazoezi na kuambulia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Future Taifa Stars.


Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume, Stars walicheza taratibu na kwa kujiamini huku vijana wa Future Taifa Stars ambayo ni timu ndogo ya taifa walionyesha wamepania zaidi.

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na na Elias Maguri ambaye alipokea pasi safi kutoka kwa Haruna Chanongo.


Stars walijitahidi kusawazisha bao hilo la Maguri lakini haikuwa kazi lahisi na hadi mwisho, ngoma ikalala wakubwa wakienda doro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic