Yanga ipo kwenye mazungumzo ya
mwisho ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa raia wa Ghana kwa katika usajili
wa dirisha dogo.
Dirisha hilo dogo limefunguliwa Novemba
15, mwaka huu ambapo Yanga imepanga kusajili mshambuliaji huyo kabla usajili
haujafungwa.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka
ndani ya kamati ya usajili ya timu hiyo, wanamuongeza mshambuliaji huyo kwa
ajili ya kukiimarisha kikosi chao kinachojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Chanzo hicho kilisema wakala kutoka
nchini huko ndiye anayeshughulikia masuala ya usajili wa mshambuliaji ambaye kabla
ya kumsajili watajiridhisha kupitia kwa mitandao ya kijamii ukiwemo wa
‘Youtube’.
“Kamati yetu ya usajili ipo kwenye
mazungumzo ya mwisho ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa raia wa Ghana
tuliyepanga kumuongeza kwenye usajili wa dirisha dogo.
“Lengo ni kukiimarisha kikosi chetu
kinachojiandaa na michuano ya kimataifa, yupo wakala tuliyempa kazi hiyo ya
kututafutia mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.
“Licha ya wakala huyo kumpa kazi hiyo,
lakini tutajiridhisha zaidi kwa kuangalia video zake za mechi alizocheza akiwa
uwanjani kwa njia ya mitandao ukiwemo wa ‘Youtube’, pia ataangaliwa na kocha
uwezo wake katika mazoezi yake kabla ya kusaini,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema wapo kwenye mazungumzo na baadhi
ya washambuliaji na wakishakamilisha watawataja hadharani.
“Kiukweli hivi sasa tupo kwenye
mazungumzo na baadhi ya washambuliaji tuliopanga kuwasajili kwenye dirisha dogo
ambao hatutawataja majina na nchi watakazotoka hadi tutakapokamilisha usajili
wao,” alisema Bin Kleb.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment