Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kimetoa
masharti kwa wachezaji wa Zanzibar Heroes kufuata sheria na taratibu iwapo
watafanikiwa kupata zawadi katika michuano hiyo kwa kutorudia kitendo cha mwaka
jana cha kugawana fedha uwanjani.
Heroes walikumbwa na mkasa wa kugawana
fedha mwaka jana katika michuano hiyo iliyofanyika nchini Uganda ambapo
walifanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu, hali iliyoleta mtafaruku kwa
wachezaji kutakiwa kuzirudisha fedha walizogawana ikiwa ni pamoja na kutishiwa
kufungiwa kuichezea timu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Rais
wa ZFA, Ravia Idarous, alisema kwa upande wao wameiandaa vyema timu hiyo na
wanachotarajia ni kuona wanafanikiwa kutwaa kombe ambalo litanogesha sherehe za
Mapinduzi na kudai kuwa iwapo watafanya vizuri wachezaji wataruhusiwa kugawana
fedha kwa kufuata taratibu.
“Tunachoangalia hivi sasa ni kombe, kuhusu
suala la fedha ni mali ya wachezaji ambapo wanatakiwa kufuata utaratibu
uliokuwepo katika kugawana.
“Nahodha anachotakiwa kukifanya ni
kumkabidhi fedha meneja wa timu kisha wagawane kwani tunachohitaji sisi ni
kombe ili liweze kunogesha sherehe za Mapinduzi,” alisema Idarous.
0 COMMENTS:
Post a Comment