December 29, 2013







Chelsea imeitandika Liverpool kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyopigwa leo jijini London.

Kutokana na ushindi huo, Chelsea imefikisha pointi 40 na kukwea nafasi ya tatu na kuiporomosha Liverpool hadi nafasi ya tano ikiwa na pointi 36.


Liverpool ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Skrtel lakini Chelsea wakasawazisha kupitia Eden Hazard katika dakika ya 17 na Samuel Eto’o akamaliza kazi katika dakika ya 34.

Katika kipindi cha pili, Chelsea ilipoteza nafasi mbili safii ikiwemo ile ya Eto’o ambazo zingeweza kuongeza wigo wa ushindi.

MATOKEO MENGINE.
Tottenham Hotspurs imeichapa Stoke City kwa mabao 3-0.
Mabao ya Spurs yalifungwa na 'Mzee wa penalti', Soldado, Moussa Dembele na Aaron Lennon.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic