| KIGGI (WA PILI KULIA) AKIWA NA MWINYI KAZIMOTO, SHOMARI KAPOMBE NA FELIX SUNZU WAKATI WOTE WAKIWA SIMBA. HII ILIKUWA MSIMU ULIOPITA, WOTE HAWA HAWAPO MSIMBAZI KWA SASA. |
Kiungo wa Simba SC, Kiggi Makasi,
ameonekana akifanya mazoezi katika Uwanja wa Azam, Chamazi kwa ajili ya
kuendelea kuiimarisha zaidi afya yake baada ya kuwa majeruhi kwa muda
mrefu.
Kiungo huyo alikuwa akisumbuliwa
muda mrefu na tatizo la goti ambalo alikwenda kutibiwa nchini India na
alipewa muda wa miezi mitatu kwa ajili ya uangalizi ili kujua
maendeleo yake kabla ya kurejea uwanjani.
Alipoulizwa Meneja
wa Azam, Alando Philipo, sababu ya kiungo huyo wa zamani wa Simba na Yanga
kufanya mazoezi na kikosi chao ambapo alidai kuwa alianza muda kidogo kufanya
mazoezi katika uwanja huo kwa kuwa anaishi jirani nao hivyo wakamruhusu.
“Kiggi anaishi jirani na hapa na kutokana
na hali yake huwa anakuja hapa kufanya mazoezi tu tena ya peke yake na si
ya kitimu kwa kuwa sio mchezaji wetu bali ni wa Simba,” alisema.
Kiungo huyo alipoulizwa kuhusu hilo
alisema: “ Mimi ni Simba jamani lakini ninakaa hapo karibu hivyo
kutokana na matatizo yangu ndiyo maana nipo hapa nafanya mazoezi tena
peke yangu tu,”alisema Kiggi.







0 COMMENTS:
Post a Comment