Kipa mpya wa Simba, Ivo Mapunda amesema
timu yake hiyo imefanya uamuzi sahihi kumsajili Donald Musoti.
Mapunda amesema beki huyo wa kati ambaye
amesaini kuichezea Simba siku moja kama ilivyokuwa kwake ni beki mzuri na wa
uhakika.
“Ni wazo zuri, ninaamini Musoti
atasaidia kwa kuwa ndiye alikuwa beki wetu tegemeo.
| IVO AKISAINI HIYO JANA JIJINI NAIROBI MBELA YA KATIBU MKUU WA SIMBA, WAKILI EVODIUS MTAWALA |
“Nafikiri hajacheza mechi chache sana za
ligi tokea misimu miwili iliyopita,” alisema Ivo.
Musoti na Ivo walikuwa wanakipiga pamoja
na kikosi cha Gor Mahia ya Kenya ambacho walifanikiwa kukipa ubingwa baada ya
kuukosa kwa zaidi ya miaka 12.
Wote wawili wametua Simba na tayari
wameishaanguka saini.
Wanatarajiwa kuanza kazi Msimbazi mara
moja chini ya kocha mpya ‘Mheshimiwa’ Logarusic.







0 COMMENTS:
Post a Comment