Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Shija Mkina, amesaini mkataba wa mwaka mmoja wakati huu wa
usajili wa dirisha dogo kuichezea JKT Oljoro ya Arusha inayoshiriki Ligi Kuu
Bara.
Katibu
Mkuu wa Oljoro, Ally Njaidi amesema kuwa lengo ya kumsajili mshambuliaji huyo
ni kuiimarisha safu ya ushambuliaji.
“Hadi
hivi sasa tumefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba, Shija ambaye
tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja, kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chetu
katika mzunguko wa pili.
“Pamoja
na kiungo wa zamani wa African Lyon, Jacob ambaye naye tumeingia mkataba wa
mwaka mmoja kama Shija, hivyo tunaamini watakiongezea nguvu kikosi chetu,”
alisema Njaidi.







0 COMMENTS:
Post a Comment