Kipa mpya wa Simba, Ivo Mapunda na beki,
Donald Musoti waliotua Simba wakitokea Gor Mahia ya Kenya, wamesababisha
kuibuka kwa vurugu jijini Nairobi.
Beki mpya wa Simba, Donald Musoti, amesema
tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita katika Uwanja wa Nyayo jijini
Nairobi wakati Gor Mahia ikiumana na Tusker katika mchezo maalum wa hisani,
ambapo Tusker iliibuka na ushindi kwa mikwaju ya penalti 5-3.
Musoti amesema mara baada ya kumalizika
kwa mchezo huo na kuwapungia mashabiki wa Gor, mashabiki hao walichukizwa na
uamuzi huo baada ya kuona uzembe wa viongozi wao kwa kuwaachia yeye na kipa Ivo
Mapunda.
Anasema mashabiki hao walianza kurusha
mawe katika magari ya viongozi wao wakati wakitoka uwanjani hapo, jambo ambalo
lilizua taharuki kubwa.
“Ilkuwa hatari sana, unajua kwanza
mashabiki hawakuwa wanajua kama tunaondoka kweli, lakini mchezo ulipokwisha,
niliwapungia mkono ikiwa ni kuwaaga, hapo ndipo walipoamini kuwa naondoka,
walichukia sana,” alisema Musoti.
Taarifa zinasema mashabiki wa Gor
hawakufurahishwa na kuondoka kwa wachezaji hao na wanaona kama viongozi wao
walikuwa tatizo.







0 COMMENTS:
Post a Comment