December 13, 2013



Kipa Ivo Mapunda na beki Donald  Musoti, wote wamesaini rasmi kuichezea Simba kwa miaka miwili.
Musoti alikuwa pendekezo la kocha Zdravko Logarusic ambaye pia alinpendekeza Mapunda.


Logarusic ambaye ni kocha wa zamani wa Gor Mahia, aliwahi kufanya kazi na wachezaji hao wawili akiwa Kenya.

SALEHJEMBE pia iliandika leo mchana na kueleza kwamba Ivo na beki huyo wamekubali kuichezea Simba na usiku wa jana wangemalizana na Simba kupitia kiongozi wake aliyekuwa Nairobi.

“Kocha ndiyo amewapendekeza, hivyo hatukuwa na namna zaidi ya kuwasainisha ili afanye kazi anayotaka,” alisema mmoja wanaohusika na usajili ndani ya Simba.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala ndiye alisimamia zoezi zima la kuwasainisha Musoti na Mapunda leo hii usiku jijini Nairobi.
Jana SALEHJEMBE iliandika na kueleza uamuzi wa Simba kufikia kwenda Kenya.
Na leo ilieleza kwamba tayari kuna ofisa mmoja wa Simba ameishatua jijini Nairobi kwa ajili ya zoezi hilo.
Ofisa huyo alikuwa ni Mtawala na amelikamilisha na Ivo aliyekuwa akiitumikia Kili Stars katika michuano ya Chalenji na Musoti watajiunga na wenzao ndani ya siku mbili kuanza mazoezi chini ya Logarusic.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic