Kwa mara ya pili mfululizo Kilimanjaro
Stars imeambuliwa kipigo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuchapwa na Zambia
katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji.
Katika mechi hiyo iliyopigwa jijini
Nairobi Kenya, Stars imefungwa mabao 6-5 ya mikwaju ya penalti na Zambia.
Timu hizo zilikwenda katika hatua ya
mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya bao 1-1, Kili stars ikisawazisha
kupitia kwa Mbwana Samatta.
Pamoja na juhudi za kutaka kushinda
mechi hiyo mapema, lakini ilishindikana hadi katika mikwaju ya penalti.
Kabla ya mechi hiyo, Kili Stars
ilikutana na kipigo chabao 1-0 kutoka kwa wenyeji Kenya katika mechi ya nusu
fainali.








0 COMMENTS:
Post a Comment