Juhudi za Jeshi la Polisi Kenya kuanza kuwasaka wachezaji wawili wa Eritrea waliozamia zimeanza.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye amesema juhudi hizo zimeanza baada ya wapo kuripoti kwa jeshi hilo.
"Tuna matumaini watapatikana na tumeawaachia wao kwa kuwa ndiyo wataalamu, lakini tunaonya hiki si kitu kizuri kwa sifa ya michuano hii," alisema Musonye.
Mapema leo wachezaji wawili wa timu ya taifa ya waliokuwa wanashiriki michuano ya Chalenji nchini Kenya, wametoweka.
Desemba, mwaka jana wachezaji 17 pamoja na dokta wa timu ya
Eritrea walitoweka na kuzamia katika mitaa ya jijini la Kampala nchini Uganda.
Lakini mwaka 2009, hali ilikuwa hivyo hivyo baada ya wachezaji
wengine kuzamia nchini katika jiji la Dar es Salaam.
Musonye alithibitisha kutoweka
kwa wachezaji hao wawili wa Eritrea.
“Walishindwa kurejea hotelini tokea jana na wenzao wamesema
watakuwa wamepotelea katika mitaa ya Kenya,” alisema Musonye.
Imeelezwa maisha katika nchi ya Eritrea yamekuwa si mazuri na
ubabe wa serikali umekuwa chanzo cha vijana wengi kuamua kutorejea kwao.
Mwaka jana Kitengo cha Haki za Binadamu cha Umoja wa Mataifa
kupitia Mkuu wake, Navi Pillay kiliilaumu serikali ya Eritrea kutokana na
uonevu na unyanyasaji.








0 COMMENTS:
Post a Comment