Kipa bora namba moja nchini Juma Kaseja,
leo aliporomosha dua wakati mwamuzi akijiandaa kuanzisha mechi ya kirafiki kati
ya Yanga iliyokuwa inawavaa KMKM ya Zanzibar.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar, Kaseja alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tokea arejee Yanga.
Wakati mwamuzi akijiandaa kuanzisha
mchezo, Kaseja aliinua mikono na kuanza kusali na alifanya hivyo kwa takribani
dakika moja, hadi pale mwamuzi alipopuliza filimbi kuanza mechi, ndiyo
akahitimisha sala yake.
Mechi ilimalizika kwa Yanga kushinda kwa
mabao 3-2, Kaseja akiwa ameanza dakika 90 za kwanza Yanga kwa kufungwa mabao
mawili.
Hata hivyo, Kocha Ernie Brandts
alimsifia kwa kuonyesha kiwango kizuri huku akisema uzembe wa mabeki
ulisababisha Yanga kuruhusu mabao hayo mawili.







0 COMMENTS:
Post a Comment