Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema ikiwezekana
ataingia mapema na kuisubiri Yanga.
Logarusic amesema anataka kuiona Yanga ikicheza angalau
mechi moja kabla ya mechi yao ya Nani Mtani Jembe, Desemba 21.
“Nataka nione mwendo wao ukoje, nikiweza nitafika mapema
zaidi kwa kuwa nataka nione mechi yote au kipindi kimoja.
“Lakini sehemu muhimu ninayotaka kuona ni namna
watakavyocheza mwanzo, kuna mambo muhimu ya kuangalia,” alisema.
Kocha huyo aliamua kubadili program yake ya mazoezi ili leo
aende akaione Yanga ambayo itakuwa mechi yake kubwa ya kwanza atakapokutana
nayo Desemba 21.







0 COMMENTS:
Post a Comment