Mshambuliaji nyota wa zamani wa Man United, Andy Cole
amesema program na promosheni zinazoandaliwa na kampuni ya simu ya Airtel
zinaweza kusaidia mabadiliko makubwa katika soka nchini.
Cole amesema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika jijini Dar.
“Kufikia mafanikio si kitu lahisi, kwanza
lazima kuwe na watu wenye ndoto na wanaotaka kuzifuata.
“Kabla ya kufikia ndoto zako lazima ujitume
kwanza. Nimeona Tanzania kuja vipaji vingi sana tokea nilipokija mwaka 2011 kwa
ajili ya Airtel Rising Star.
“Hizi program za Airtel ni sehemu ya
changamoto kusaidia kwenda juu, inawezekana kabisa Tanzania ikawa na mchezaji
Premiership na akafanikiwa,” alisema.
Mkali huyo wa mabao England, kesho atakuwa Karume kugawa
mipira kwa watoto na baada ya hapo, atasepa hadi Coco Beach ambako ataangalia
mechi pamoja na wadau.
Mechi atakayoangalia ni kati ya Man U dhidi ya Aston Villa.







0 COMMENTS:
Post a Comment