Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic
ameendelea kulia kwamba hapendi kuzungumia wachezaji wa timu nyingine.
Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Croatia, Logarusic
amesisitiza kwamba hana mpango hata kidogo kutaka kuzungumzia wachezaji wa timu
nyingine kama ilivyoripotiwa na gazeti la Mwanaspoti.
“Nimesoma na nimezungumza na baadhi ya
rafiki zangu, kwamba mimi siwezi kuzungumzia wachezaji wa timu nyingine.
“Hakikuwa ni kitu kizuri kabisa,
kunisingizia maneno yale. Nimesomewa kwamba ningepewa Yanga basi ningewafukuza
mabeki wote, si kweli.
“Nimekasirika sana, nilitamani nirudi
Tanzania kufafanua suala hilo,” alisema.
Baada ya gazeti hilo kuandika, siku
iliyofuata taarifa zilizagaa kwenye mitandao zikieleza kukasirishwa kwa kocha
huyo.
Logarusic alimtumia ujumbe msemaji wa
zamani wa Simba, Ezekiel Kamwaga alilalama kuhusiana na habari hiyo.
Kamwaga akaitundika kwenye ukurasa wake wa
Facebook ingawa mara baada ya watu kuanza kuandika wakiliponda gazeti hilo la
michezo, akaitoa.







0 COMMENTS:
Post a Comment