December 9, 2013





Makocha wawili wakongwe wa Ligi Kuu Bara, Mrage Kabange na Mohamed Kampira, wameitabiria mazuri Kilimanjaro Stars, wakidai itatinga fainali na kutwaa ubingwa wa Chalenji mwaka huu.


Stars iliwafurahisha mashabiki wa soka nchini baada ya kuifunga Uganda kwa penalti 3-2 na kutinga nusu fainali ya Chalenji ambapo kesho Jumanne itavaana na Kenya katika michuano michuano hiyo inayoendelea nchini Kenya.

Kabange ambaye ni Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, amesema baada ya Stars kuwafungashia virago waliokuwa mabingwa watetezi, hakuna tena kipingamizi kikubwa kwao.

“Kili imeifunga timu ngumu ukilinganisha na Kenya ambao ni wenyeji, matumaini makubwa ya kutinga fainali yapo kutokana na timu yetu kuwa na mchanganyiko wa wachezaji wa rika tofauti ambao nina imani watapigana kuhakikisha wanarudi na kombe.

“Kwa jinsi kikosi kilivyokomaa kimashindano huwezi kuwa na hofu yoyote, katika safu ya ushambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wametengeneza kombinesheni ya hatari ambayo muda wowote unaweza kushangilia goli,” alisema Kabange.

Kwa upande wake Kampira ambaye ni Kocha Mkuu wa Mgambo JKT, alisema kikosi cha Stars kipo katika morali ya ushindi kwa sasa baada ya kuitoa Uganda.

 “Nawaomba Watanzania wawe na imani na timu yao kwa kuwa wachezaji wote walioko Kenya wanajua wanachofanya na wanatambua wadau na mashabiki wa soka wako nyuma yao na wanahitaji ushindi katika mchezo unaofuata,” alisema Kampira.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic