December 9, 2013





Uongozi wa Kagera Sugar, umethibitisha kuwa katika hatua za mwisho kumalizana na aliyekuwa beki wa kati wa Yanga, Chacha Marwa, ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Ligi Daraja la Kwanza, Ndanda FC ya Mtwara.


Kagera imekuwa ikihaha kumpata beki wa kati mwenye uzoefu mkubwa tangu kuumia kwa Amandus Nesta msimu uliopita.

Mrage Kabange, alisema: “Kila kitu kimekamilika kwa upande wa timu, tumebakiza makubaliano yetu na mchezaji mwenyewe, japo tayari tumeteta naye, sema hatujamalizana kwenye kipengele cha maslahi. Naamini kufikia Desemba 10 (kesho), kila kitu kitakuwa wazi.”

Kagera Sugar ni moja ya timu ambazo zimekuwa zikitoa ushindani wa kutosha kwenye Ligi Kuu Bara na katika mzunguko wa kwanza imemaliza ikiwa kwenye nafasi ya tano, ikiwa na pointi 20 ambazo ni nane pungufu ya vinara, Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic