Mabao mawili ya Emmanuel Okwi na moja la
Hamis Kiiza yametosha kuwaondoa mashindanoni Ertirea.
Uganda, The Cranes imeibabua Eritrea kwa
mabao 3-0 katika mechi ya michuano ya Chalenji iliyopigwa jijini Nairobi, Kenya.
Okwi ndiye alikuwa wa kwanza kuifungia
bao kupitia pasi ya Sserunkuma, Kiiza akafunga la pili kwa mkwaju wa penalti
baada ya Sserunkuma kuagushwa.
Sserunkuma alitoa pasi nyingine kwa Okwi
ambaye alimalizia kazi na kuwafanya vijana wa Micho wafuzu kwenye hatua ya robo
fainali wakitokea kundi C.








0 COMMENTS:
Post a Comment