December 2, 2013

AMAVUBI (TWITE NA KAREKEZI HAWAKUWEMO KATIKA KIKOSI KILICHOSHIRIKI CHALENJI)

Rwanda imefungwa mechi ya pili mfululizo katika michuano ya Kombe la Chalenji, maana yake haina nafasi ya kusonga mbele.
Michuano hiyo inaendelea nchini Kenya na timu za Zanzibar na Bara ni kati ya zinazoshiriki na kila moja imeonja ushindi.

Leo Rwanda maarufu kama Amavubi imefungwa kwa bao 1-0 na Sudan ikiwa ni mara ya pili baada ya kupoteza kwa idadi hiyo dhidi ya Uganda.
Juhudi za nahodha, Haruna Niyonzima aliyeonekana kuhaha uwanja mzima baada ya Salah kuifungia Sudan bao, hazikuzaa matunda.

Mechi ilikuwa nzuri lakini Sudan walionekana kujipanga vizuri kiufundi na kuizuia Amavubi kwa dakika zote 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic