Hatimaye beki
kisiki wa Simba, Joseph Owino amerejea nchini.
Owino raia
wa Uganda ametua nchini jana akitokea kwao Uganda.
Awali Kocha
Logarusic alilalama kuhusiana na kuchelewa kwa wachezaji watatu, Amissi Tambwe,
Owino na Gilbert Kaze ‘Demunga’.
Kocha huyo
ameishatishia kuwakata mshahara na tayari amesema atapeleka pendekezo lake
kwenye kamati ya ufundi na nidhamu.
Hata hivyo,
Owino alionekana ni mwenye furaha na aliye tayari kuanza kazi kujiandaa na
mechi ya Nani Mtani itakayopigwa Novemba 21.









0 COMMENTS:
Post a Comment