![]() |
| AMROUCHE, ALIYEBEBA KOMBE AKIWA NA MSAIDIZI WAKE |
Kocha Mkuu ya Kenya, Adel Amrouche
amesema ametwaa Kombe la Michuano ya Chalenji, si kwa bahati.
Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili
ya Algeria amesema pamoja na kutokuwa na maandalizi ya kutosha sana, lakini
kujituma kwa wachezaji na benchi la ufundi, kumezaa matunda.
“Tulitaka kulitwaa kombe hili, kila
mmoja alijituma na tulifanya kazi kwa kutaka kutimiza malengo.
“Tulijua Wakenya wote walisubiri
mafanikio yetu nasi tukapambana vilivyo,” alisema Amrouche.
“Tuliweza kuzifunga timu zote bora
ikiwemo Tanzania na Sudan, mwisho sisi ndiyo tumekuwa bora kuliko wengine.
“Nawashukuru wachezaji wangu, watu wa
benchi la ufundi na wote waliojituma kwa ajili ya mafanikio kwa Harambee Stars,”
alisema Amrouche aliyeonekana kuwa kocha bora zaidi katika michuano hiyo.








0 COMMENTS:
Post a Comment