December 29, 2013




Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema litaisaidia Simba kudai fedha zake dola 300,000 kwa Etoile du Sahel.

TFF imesema isaidiana na Simba kwa kuwa inajua haijalipwa hata senti baada ya Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage kwenda kumuuza Okwi nchini Tunisia, halafu akarejea nchini hata bila senti tano.
TFF kupitia kamati yake ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imesema inafahamu kuwa klabu ya Simba bado haijalipwa na itasaidia kufuatilia FIFA fedha za mauzo ya mchezaji huyo.

Hii si mara ya kwanza kuahidi kusaidiana na Simba kufuatilia fedha za Okwi ambazo tayari zinaonekana ni kizumbumkuti.
Kwani Etoile Du Sahel wanaodaiwa na Simba tayari mchezaji hayuko mikononi  mwao.

Mbaya zaidi ni hivi, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ndilo limeithinisha auzwe Yanga.

Katika mauzo, Etoile ya Tunisia haijapata hata senti, maana yake itakuwa vigumu nao kulipa.
Hivyo inawezekana fedha hizo hata kama TFF itaisaidia Simba, zitaendelea kudaiwa bila ya mafanikio.


2 COMMENTS:

  1. MIMI SWALI LANGU NI MOJA TU HIZO 300M KALIPWA NANI, AU NI UBABAISHAJI WA AFRICA

    ReplyDelete
  2. WEWE UMEONA WAPI MWENYEKITI WA CLUB AKAUZA MCHEZAJI HUU MWINGINE UBABAISHAJI SIMBA HAINA ACCOUNTANT KWANI,RAGE WEWE NI MWIZI UMEIBA PESA ZA SIMBA HILO HALINA MJADALA KAMA HUJAIBA NA HUJA POKEA PESA BASI OKWI HAWEZI KUA MCHEZAJI YANGA MAANA IKO NYEUPE HIYO,KAMA TIMU YA TUNISIA HAKUTOA KIBALI CHA KUUZWA OKWI BASI HICHO KIBALI CHA YANGA NA FUFA NI FAKE NA YANGA WAMEIBIWA PESA ZAO

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic