Pamoja
na kwamba hakushiriki hata kidogo katika maandalizi ya mechi ya Simba wakati
ikiivaa Yanga katika nani Mtani Jembe na kushinda bao 3-1, Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), limemtangaza Ismail Aden Rage ndiye Mwenyekiti halali wa klabu
hiyo.
Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji imemtaka kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu wa taratibu za klabu ya
Simba.
Kamati
imebaini upungufu kadhaa wa kisheria kwenye uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya
Simba uliofanywa Novemba 18, 2013 kwa kumsimamisha Mwenyekiti wao.
Upungufu huo ni pamoja na ukiukwaji
wa Ibara ya 33 ya Katiba ya Simba juu uitishaji wa mkutano, ajenda ya
kumsimamisha Mwenyekiti kuwasilishwa kwenye kikao kwa utaratibu wa mengineyo.
Changamoto
nyingi zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti huyo zingeweza kupatiwa ufumbuzi kwa
kutumia Ibara ya 16(2) ya Katiba ya Simba.
Hivyo,
agizo za Rais wa TFF, Jamal Malinzi kumtaka Mwenyekiti wa Simba aitishe mkutano
lipo palepale. Pia Mwenyekiti ametakiwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya
Makamu Mwenyekiti kwa kuzingatia Katiba ya klabu hiyo.
Katika
mkutano huo wa kujaza nafasi, ndiyo utakaojadili mgogoro kati ya Mwenyekiti na
Kamati yake ya Utendaji. Nafasi hiyo kwa sasa inakaimiwa na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya klabu hiyo, Joseph Itang’are baada ya Geofrey Nyange aliyekuwa akiishikilia
kujiuzulu.
TFF
inakumbusha wanachama wake wote (vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za
Ligi Kuu) kuzingatia Katiba zao. Kamati pia imegundua ukikwaji wa maadili
katika suala hili, hivyo, litapelekwa katika kamati husika.
Kwa
vile maslahi ya TFF ni kuona mpira wa miguu unachezwa kwa utulivu,
itazikutanisha pande husika wakati wowote kuanzia sasa.








0 COMMENTS:
Post a Comment