December 9, 2013





Kikosi cha Kilimanjaro Stars kimepata ofa kubwa baada ya kupewa zawadi nono ya mamilioni na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
 
Zawadi hiyo imetolewa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi amsema tayari alishazungumza na nyota wa timu hiyo kupambana na endapo watafanikiwa kuchukua ubingwa, kikosi hicho kitagawana zawadi ya bingwa, kiasi cha dola 30,000, sawa na Sh milioni 48.

Malinzi amesema ofa hiyo haitaishia hapo. Wakishika nafasi ya pili watagawana dola 20,000, sawa na Sh milioni 32 na wakiambulia nafasi ya tatu watapata dola 10,000 (Sh milioni 16).

“Nawapongeza sana Stars kwa ushindi huo lakini wanatakiwa kujua kwamba safari bado ndefu, Watanzania wanataka ushindi kwa kuchukua ubingwa, hivyo wanatakiwa kupambana na kuhakikisha wanalileta taji hapa nchini,” alisema Malinzi.

“Nilishawaeleza mapema katika mkutano wangu na timu hiyo tukiwa kule Nairobi wakati nikihudhuria mkutano wa Cecafa kwamba kama wakifanikiwa kushika nafasi tatu za juu kuanzia bingwa, mshindi wa pili na ile ya watatu, watachukua fedha zote na kugawana wao, mimi sitaki kuziona hizo fedha TFF, ni za kwao, kazi kwao kupambana sasa.”

Tayari kikosi hicho kimeshatinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Chalenji inayoendelea jijini Nairobi nchini Kenya ambapo kesho kitavaana na Kenya.
SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic