Timu ya
Seeb Club ya Oman imeendelea kutesa katika ligi kuu ya nchi hiyo.
Seeb
anayoifundisha Mtanzania, Manyika Peter imefanikiwa kuwachapa vigogo Fanja kwa
bao 1-0.
Manyika
ambaye ni kocha wa makipa wa timu hiyo amesema baada ya kushinda mchezo huo mwishoni mwa wiki, sasa wanafunga safari
kwenda mkoa mwingine.
“Tunasafiri
kwenye mkoa mwingine kuendelea na ligi ingawa kutakuwa na ushindani mkubwa,
unajua mnaposhinda dhidi ya timu kongwe kama hizo basi lazima timu mnayocheza
nayo inapania sana.
“Lakini
tuna kikosi kizuri na tumejiandaa vilivyo kwa ajili ya kucheza vizuri na
kushinda,” alisema Manyika kutoka nchini Oman.
Wakati akiwa mchezaji, Manyika aling'ara akiwa na Yanga, Mtibwa Sugar, Kili Stars na Taifa Stars.










0 COMMENTS:
Post a Comment