| BAHANUZI (KULIA) AKICHUANA NA JAVU |
Mshambuliaji wa Yanga Said Bahanuzi bado
anahitajika nchini Malsyia baada ya klabu nyingine kuonyesha nia ya kuhitaji
huduma yake.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto,
amesema Bahanuzi alikuwa nchini humo siku tano zilizopita, akipelekwa kwa lengo la majaribio katika klabu ya
Terrenganu FA, inayoshiriki ligi kuu nchini, lakini klabu nyingine ya T Team
imejitokeza katika nia ya kumuwania mshambuliaqji huyo wa zamani wa Mtibwa
Sugar.
Kizuguto, amesema awali T Team ilimuona
Bahanuzi wakati ikicheza mchezo wa kirafiki na Terrengan, lakini ilitaka
mshambuliaji huyo kurudi nchini kwanza kabla ya kupewa mualiko mpya,
utakamrudisha Malsyia kumalizia hatua ya mwisho kabla ya kusajiliwa.
“Ikumbukwe kuwa, Bahanuzi alishafanya
mjaraibio na Terrenganu lakini wakati akiwa huko, klabu hiyo ilicheza mchezo wa
kirafiki na hiyo T Team, ambao nao waliopoonyesha kumuhitaji mchezaji wetu,
katika hilo wakaona kwanza amalize majaribio ya sasa na akirudi huku watamtua
mualiko mwingine kurudi huko,” alisema Kizuguto.
“Kwasasa Bahanuzi tunaye hapa kutokana
ni mchezaji ambaye yupo kwenye mipango yetu na kama T Team wakituma huo mualiko
tutampa ruhusa ya kurudi huko haraka kutafuta bahati yake ya kucheza soka la
kulipwa.







0 COMMENTS:
Post a Comment