Kiungo wa zamani wa Yanga, Abdi Kassim, jana aliikoa timu
yake ya UITM FC baada ya kufunga bao la kusawasisha katika dakika ya 90.
Kikosi cha timu yake kilikuwa kimetota baada ya wapinzani wao JDT II kupata bao mapema na ilionekana kama ndiyo mambo yamekwama.
Lakini bao la kiufundi la Kassim maarufu kama Babi,
liliisaidia timu yake hiyo kutoka na pointi moja uwanjani katika ligi ya
Malaysia.
Tayari Babi, amekuwa tegemeo katika kikosi cha timu hiyo na
wamekuwa wakimtumia kama mchezesha timu.
0 COMMENTS:
Post a Comment