January 29, 2014


Uuzwaji wa tiketi za elektronik umezua tafrani mjini Tanga kwa kuwa mashabiki wa soka wanaonekana kutoelewa.

Tiketi hizo ni za Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Coastal Union dhidi ya wageni wake, mabingwa watetezi Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwaji mjini hapa.


Mashabiki wanaonekana kutofurahia utaratibu wa kwenda katika benki ya CRDB na kununua tiketi hizo, huku utaratibu ukionekana kuwa tofauti na ule wa awali.

Kwanza kwa mashabiki kutoka mikoani wamekuwa wakilalamika kwa kuwa wanalazimika kuzifuata tiketi kwenye matawi ya CRDB yaliyo Raskazone na Usagara ambako ni mbali na uwanjani.


Wengine hawayajui maeneo hayo, hivyo wanalazimika kuingia gharama ya usafiri ili kwenda kwenye maeneo hayo jambo wanaloamini ni usumbufu kwao.

Lakini imekuwa lahisi zaidi kama wakifika katika maeneo hayo kwa kuwa uuzwaji wa tiketi unakwenda vizuri na haraka, hivyo hata kama foleni ni ndefu lakini inatembea haraka.
KIZUGUTO ALIKUWEPO PIA


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic