Siku moja tu baada ya kuisaidia timu yake ya Manchester United,
kiungo nyota Juan Mata ameshinda akizunguka kwenye mitaa ya mji wa Manchester
akitafuta nyumba.
Mata ,25, aliongozana na mpenzi wake pamoja na madalali kutafuta
nyumba ya kuishi katika eneo maarufu la Chesire katika mji huo.
Eneo la Cheshire linawavutia nyota wengi sana wakiwemo wa Manchester
United na Manchester City na ilionekana huenda Mata naye akaishi eneo hilo.
Wachezaji wengine wanaoishi katika eneo hilo maarufu ni pamoja na mates
Wayne Rooney, Nemanja Vidic, Nani, Patrice Evra, Ashley Young wa Man United,
pia David Silva na Joleon Lescott wa Man City.
Mata amejiunga Man United kwa kitita cha pauni milioni 37.1
akitokea Chelsea na mechi yake ya kwanza akiwa na timu hiyo ameisaida United
kushinda 2-0, akitoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Young baada ya van
Persie kutangulia kufunga la kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment